Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Mhagama (mwenye nguo nyekundu) akimfariji
Mwenyekiti wa Bunge Bi. Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge kuahirishwa
kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa. Kulia ni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary Nagu na kushoto ni wabunge James
Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki usiku wa
kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake zimetangazwa
wakati bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya afya hivyo kupelekea
bunge hilo kuahirishwa hadi tarehe 4 mwezi huu.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki (kushoto)
akitoka nje ya ukumbi wa bunge akiwa ameambatana na wabunge Bi. Mary Mwanjelwa
na Rita Kabati baada ya bunge hilo kuahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge wa
Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt Seif Rashid akiwasilisha bungeni makadirio
ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/2016 leo mjini
Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Dodoma.

No comments:
Post a Comment