Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BOHARI YA KUHIFADHI MAFUTA YA GBP MKOANI TANGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Jeti ya kupokelea mafuta na Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika eneo hilo baada ya kukagua kituo hicho cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, mkoani Tanga jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoizana na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya GBP, wakati akielekea kukagua Bohari ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya GBP, alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya GBP, Badar Seif Sood, (wa pili kulia) wakati alipotembelea Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, kwenye ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika eneo hilo, akiongozana na Mkurugenzi wa ya GBP, Badar Seif Sood (kushoto), Waziri wa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge na baadhi ya viongozi, baada ya ukaguzi wa Bohari ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya GBP, mkoani Tanga jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya GBP, Badar Seif Sood, baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, jana mkoani Tanga. 
***************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania amefanya ziara Tanga kukagua Bohari ya kuhifadhi mafuta na jety ya kampuni ya GBP Tanzania Ltd Makamu wa Rais akifuatana na
Waziri ofisi ya makamu wa Rais mungano,
Waziri ofisi ya Makamu wa rais mazingira,
Naibu waziri ofisi ya Makamu wa Rais,
Katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Rais,
Katibu mkuu Wizara ya uchukuzi,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Mkuu wa mkoa wa Dodoma,
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Bandari,
Mkuu wa wilaya ya Tanga ,
Mstahiki meya wa Tanga,
Viongozi wa vyama

Ziara na ukaguzi wa Bohari na jety ya GBP ni kufuatia uamuzi wa Serikali Tanga kuwa Bandari ya pili ya upokeaji wa mafuta kupitia BPS (Bulk Procurement System)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.