Habari za Punde

*MAREHEMU EUGEN ALIVYOAGWA NA WABUNGE MJINI DODOMA JANA

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Martha Mlata akiimba kwa hisia wimbo wa maombolezo kwenye  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga iliyofanyika leo katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma wakati wa  shughuli ya kuaga mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa.
 Baadhi ya Wabunge wakiwa kwenye hali ya majonzi mara baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu  Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma jana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.