Habari za Punde

*KIMENUKA DODOMA, WAFUASI WA LOWASSA WALIANZISHA WAFUNGA BARABARA, WATAWANYWA NA POLISI

 Wanaodaiwa kuwa ni Wafuasi wa aliyekuwa Mgombea Urais Edward Lowassa, aliyekatwa katika hatua ya Tano Bora, wakitimua mbio wakati wakitawanywa na Gari la Polisi walipokuwa wakijaribu kuandamana huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kumsifu na kumtukuza mgombea wao, wakiwa wamefunga barabara ya mbele ya Ofisi za CCM Makao Makuu mjini Dodoma. Wafuasi hao bado wapo mpaka muda huu wakiendelea kuimba kwa sauti huku wakidhibitiwa na Polisi kutosogelea eneo la Ukumbi huo wa mikutano.
 Katika harakati hizo ilibidi askari hao kutumia Mbwa ili kuwatawanya wafuasi hao huku, wanahabari nao wakiwa bize kupata matukio.

Polisi wakiwa Doria eneo la tukio.....
 Mbwa wakiendelea kuwatawanya wafuasi hao...
 Mbwa wakitawanya wafuasi hao....
 Umati wa watu wakiwa wamekusanyika nje ya Ofisi hizo wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Wanahabari wakinasa matukio....
 Wafuasi hao wakikimbia huku wakiimba nyimbo mbalimbali katikati ya barabara.
 Mama na mwanawe wakitimua mbio kujiokoa wakati wakitawanywa wafuasi hao....
 Umati wa watu ukiwa umefunga barabara...
 Wafuasi hao wakiimba nyimbo mbalimbali.....
 Umati wa watu ukiwanje ya Ofisi hizo.....
 Wafuasi hao wakiendelea kuserebuka huku wakiimba....
 Wafanyabiashara wakihamisha biashara zao kukimbi eneo hilo lililogeuka 'Soweto' kwa muda...
Wengine wakifungasha biashara zao tayari kuondoka eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.