Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa kwa siku za jumamosi na jumapili katika viwanja nane tofauti nchini ikiwa ni mzunguko wa tatu tangu kuanza kwa ligi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Leo Jumamosi mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, watakuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Chama la Wana Stand United watawakaribisha Wana Kimanumanu African Sports kutoka Tanga, katika dimba la Kambarage mjini Shinyanga.
Jijini Mbeya kutakua na mpambano wa wenyeji wa mji huo (Mbeya Derby) kati ya Tanzania Prisons watakapokuwa wakipambana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini humo, huku Maafande wa Mgambo Shooting wakiwakaribisha Wana Lizombe Majimaji FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo minne kuchezaw, Simba SC watawakaribisha Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Mwadui FC wakiwa wenyeji wa Azam FC katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
Wakata miwa wa Turiani Mtibwa Sugar watawakaribisha Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Toto Africans katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
*U15 WALIOKWENDA MAZOEZI ORLANDO PIRATES WAREJEA
Kufuatia safari ya vijana watano wa U15 Asaad Ali Juma, Maziku Aman, Issa Abdi, Kelvin Deogratias, Athumani Maulid waliokwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Orlando Pirates kufuatia mwaliko uliotolewa na TFF na klabu hiyo, safari hiyo ilikamilika na vijana wamerejea nyumbani. Fuata link chini kwa taarifa zaidi
*FDL KUTIMUA VUMBI KESHO
Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao. KUSOMA ZAIDI BOFYA LINK HIYO CHINI
No comments:
Post a Comment