Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird (wa pili kushoto), wakisaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Muwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird wakibadilishana Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II, Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine wakifuatilia maelezo ya Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bi. Bella Bird. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Makubaliano yaliyofanywa kati ya Tanzania na Benki ya Dunia ya ili kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akibadilishana mawazo na Mratibu Maendeleo ya Sekta Binafsi na SAGCOT kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kumaliza kusaini Hati ya Makubaliano itakayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya Sh. Bilioni 440 kwa ajili ya mradi wa Tasaf II. Tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Wizara Jijini Dar es salaam
********************************************
*SERIKALI
YASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA BILIONI 440 NA BENKI YA DUNIA
Na
Benny Mwaipaja, WFM
Serikali kupitia
Wizara ya Fedha na Mipango imesaini hati ya makubaliano na Benki ya Dunia
itayoiwezesha Tanzania kupata nyongeza ya fedha katika mradi wa Tasaf kiasi cha
Shilingi Bilioni 440.
Hati hiyo ilisainiwa
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mwakilishi
Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, Dar es
Salaam, leo, Juni 23, 2016.
Akiongea wakati wa
kusaini hati hiyo Dkt. Likwelile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika
mradi wa Tasaf II kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini kukuza kipato chao
kupitia ajira za muda zitakazowawezesha kupeleka watoto shule na kuwapatia
huduma za afya.
Aliongeza kuwa katika
mwaka wa fedha 2015/2016 Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imefanya
kazi kubwa iliyowezesha miradi kumi kupitishwa ambayo ina thamani ya Shilingi Trilioni
1.9.
"Miongoni mwa
miradi iliyopata ufadhili ni pamoja na mradi wa kuboresha mazingira ya biashara
uliopata shilingi Bilioni 168, mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA), uliopata
Shilingi Bilioni 440" Aliongeza Dkt. Likwelile
Aidha, alisema kuwa
Serikali inaendelea na majadiliano na Benki hiyo kwa ajili ya kuboresha Bandari
ya Dar es Salaam, ambapo kiasi cha dola Milioni 600 zimetengwa kwa ajili ya
kazi hiyo.
Dkt. Likwelile
ameishukuru Benki ya Dunia kwa mchango wake mkubwa na kusema kuwa Serikali
itahakikisha kuwa inazisimamia taasisi zinazotekeleza miradi hiyo ili ziweze
kutumia fedha hizo vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird, amepongeza juhudi za Serikali
ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa
na kuweka mazingira rafiki kwa sekta binafsi.
Aliongeza kuwa sekta
binafsi ndizo zinatoa ajira kwa wingi na kusaidia kuchangia katika kuongeza
mapato ya Serikali.
Ameahidi kuwa Benki
yake itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuiwezesha kufikia malengo yake ya
kiuchumi na kijamii kwa faida ya wananchi wake.
No comments:
Post a Comment