Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa
Majengo nchini (TBA) Bw. Elius Mwakalinga wa kwanza kushoto akiwaongoza
wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya usafi jijini Dar es salaam katika
kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma.
Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) wakishiriki katika kufanya usafi jijini Dar es salaam ili kuadhimisha kilele cha wiki ya utumishi wa Umma. Picha na Ally Daud-Maelezo
********************************************
Na
Ally Daud-Maelezo
Wakala wa Majengo nchini (TBA)
wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.6 sawa na asilimia 43 kwa
kipindi cha miezi mitatu ambayo wapangaji wa nyumba hizo kushindwa kumalizia madeni wanayodaiwa
Akizungumza hayo katika kilele cha
kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma nchini Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw.
Elius Mwakalinga amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya kiasi hiko cha fedha
kutoka kwa wateja wao waliowapangisha majengo na bado wanaendelea kukusanya
mpaka watakapomaliza.
“Kutokana na mkakati wa kukusanya
mapato na kutoa huduma bora kwa wateja wetu tumefanikiwa kukusanya shilingi
bilioni 2.6 katika kipindi cha miezi mitatu tuliyowapa wateja wetu kuweza kukamilisha malipo hayo” alisema Bw.
Mwakilinga
Mbali na hayo Bw. Mwakilinga amesema
kuwa wameamua kutumia siku hiyo kufanya usafi kwenye makazi ya watumishi wa
umma na wakazi wengine ili kuweka mazingira bora kwenye miradi yao na jamii
nzima kwa ujumla.
“Siku ya leo tumeamua kuitumia kufanya
usafi kwenye maeneo ambayo tumeweka miradi yetu kwa watumishi wa umma pamoja na
mazingira mengine ili kuepuka na magonjwa yasababishwayo na uchafu” alisisitiza
Bw. Mwakilinga.
Aidha Bw. Mwakilinga amesema wanampango
wa kupanua wigo wa huduma yao kwa kuwapangisha watumishi wa umma ambao wanastaafu waendelee kukaa
kwenye nyumba hizo ili wasipate shida mara baada ya kustaafu.
Mbali na hayo Mkurugenzi Mtendaji huyo
amesisistiza kuwa wataendelea na
utaratibu wao wa kukusanya kodi na
kuchukua nyumba zao kwa wale ambao
wamekaidi amri yao ya kutolipia kodi nyumba hizo ili wapewe wengine ambao wana
huitaji .
Wiki ya utumishi wa Umma
imeadhimshwa kwa kila taasisi ya
kiserikali kusikiliza na kutatua kero zinazowapata wateja wanaoutumia huduma za
taasisi husika ili kuipeleka nchi katika utendaji bora na mafanikio kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment