Habari za Punde

*JAMAL MNYATE ATUA SIMBA KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

 Mchezaji Jamal Mnyate (pichani juu) akiwa katika moja ya mchezo wakati akiwa na timu ya Mtibwa Sugar.
********************************************
Na Zainab Nyamka, Dar
MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Jamal Mnyate (pichani) amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba sc Msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara ingawa ameweka wazi kuwa kuchelewa huko ni kwasababu kuna mambo walishindwa kufikia muafaka.

"Siku chache zilizopita nilikuja Dar kusaini, lakini tulishindwa kukubaliana na nikarudi Nyumbani Morogoro, nimekuja Dar jana nimesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufikia makubariano. Kwahiyo kila kitu tayari na nimerudi zangu Morogoro, ila kila kitu kiko poa kabisa na Simba",amesema Mnyate

Usajili wa mchezaji huyo umeonekana kuwavutia mashabiki wengi wakati tetesi zikitawala kwamba atatua Msimbazi, wengi wao wamesifia na kusema anaweza kusaidia kwenye kikosi cha Simba

Simba pia imemsajili mlinzi wa Mwadui, Emmanuel Simwanza, ingawa kamati ya Usajili ya klabu hiyo inasema mambo yao ni kimya kimya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.