Habari za Punde

*NAIBU WAZIRI WA NCHI MAZINGIRA NA MUUNGANO AWAZAWADIA WASHINDI WA TAMASHA LA AJIRA NA UJASIRIAMALI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina Akikabidhi Zawadi kwa Washindi  Wajiojishindia Zawadi Mbalimbali Kutoka Kampuni ya Huawei Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Mkoani Mbeya.
Chuo kikuu cha Mzumbe jijini Mbeya kiliendesha kongamano la Ujasiliamali ambalo lilihuishwa na shindano la “badirika kwa vitendo” ambapo Wanafunzi sita walijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mikononi toka kampuni ya Huawei. 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina Katika Picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba na Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG group Imani Kajula na washindi waliojinyakulia Zawadi Mbalimbali.Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba  Ambaye naye alitoa Mada Mbalimbali Namna ya Kukabiliana na Changamoto ya Ajira Hapa NchiniAfisa Mtendaji Mkuu waEAG group Imani Kajula Akitoa Mada kwenye Tamasha La Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Mkoani Mbeya
Katika hafla hiyo ya usiku, Wanafunzi hao sita Elisha Tullo, Nelson Mkolozi, Goodlove Msigwa, Agness Ngusa, Leornard Meshack walieleza walichojifunza na jinsi watakavyotumia ujuzi wao. Mshindi wa kwanza alikuwa ni Elisha Tullo na wa pili alikuwa Goodlove Msigwa.
Washiriki wa Tamasha Hilo wakisikiliza Kwa Makini Mda Mbalimbali Zilizowasilishwa  Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya Kuona picha zaidi za washindi na usiku wa wajasiliamali tembelea  Facebook page www.facebook.com/Faharinews

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.