Habari za Punde

*BALOZI WA CHINA NCHINI DKT. LU YOUQING, AUNGANA NA WATANZANIA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBI

BALOZI wa China nchini Tanzania, Dkt. LU Younqing, akitolewa damukwenye maabara kuu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH), wakati wa siku ya uchangiaji damu nchini, Juni 14, 2016. Balozi huyo aliongoza maafisa katikaofisi yake na madaktari wa Kichina wanaojitolea kwenye hospitali hiyo ili kuunga mkono juhudi za kupunguza upungufu wa damu.(PICHA NA KVIS MEDIA/KHALFAN SAID)
******************************************
NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID
BALOZI wa China nchini Tanzania, Dkt. LU Youqing, leo Juni 14, 2016 ameungana na Wataznania kujitokeza kuchangia damu kwenye Hospitaliya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam, wakati taifa likiwa limeitangaza siku hii ya leo kama siku ya taifa ya kuchangia damu.
"Nimekuwa nikisoma kwenye magazeti Muhimbili yakabiliwa na upungufu wa damu, ndio maana leo nimekuja kuchangia damu." Alisema Balozi huyo wakati akinywa chai ya rangi baada ya kutolewa damu. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu aliyetolewa damu hupaswa kunywachai ya rangi au kinwaji chochote baridi kama juisi au soda.
Balozi huyo hakuchangia damu peke yake bali maafisa wa ubalozi aliofuatana nao, Bw.XU Jingchum kutoka idara ya Diplomasia ya umma na habari, na Bw.Song. Hali kadhalika madaktari kadhaa wa Kichina wanaojitolea pale hospitali ya Taifa Muhimbili nao walijitolea damu.
Baada ya kutolewa damu Balozi huyo mcheshi, alikabidhiwa cheti na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bw. Makwaia Nakani, kama isharaya kutambua mchango wake wa damu. Baada ya kukabidhiwa balozi huyo alikaribishwa kwa chai ya rangi.
Awali Balozi huyo alifanya mazungumzo mafupi na uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), ambayo jengo lake lilijengwakwa msaadawa serikali ya China. Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohammed Janabi, aliishukuru China kwa msaada wake katika sekta ya Afya na kutolea mfano madaktari wa China ambao kwa sasa wanafanya kazi kwenye Hospitali hiyo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani alimpongeza balozi huyo wa China kwa niaba ya nchi yake kwa msaada mkubwa ambapo China imekuwa ikiisaidia Tanzania katika maeneombalimbali ikiwemo sektaya afya. "Timu ya madaktari kutoka China, wamekuwa wakifanya kazi kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili tangu mwaka 1968 bila kuchoka siotu kutibuwagonjwa bali pia kuleta utaalamu zaidi kwa wataalamu wetu." Alisema Makwaia. 
Balozi Dkt. LU, akitolewa damu huku waandishi wa habari wakiwa "bize" katikakutekeleza wajibu wao
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, MHN, Bw. Makwaia Makani (kulia), akimkabidhi cheti cha shukrani Balozi Dkt. LU baada ya kutoa damu
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kidiplomasiana habari wa Ubaloziwa China, XU Jingchun, naye akitoa damu
Balozi wa China Dkt. LU(Kulia), akimuonyesha alama ya dole, Mtanzania aliyejitokea kuchangia damu kwenye maabara kuu ya MNH
Madaktari wa Kichina wanaofanya kazi kwenye hospitali ya taifa Muhimbili, wakichangia damu, (wapili kushoto) ni mkurugenzi wa idara ya Uhusiano wa kidiplomasia na habari wa ubalozi wa China hapa nchini, XU Jingchun
Muuguzi Mkuu daraja II wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH), Lucy Warioba, akitazama ujazo wa damu wakati zoezi la utoaji damu likiendelea kwenye maabara kuu ya Hospitali
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Profesa Mohammed Janabi (kushoto), akizungumza jambo wakati balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing alipotembelea kwa nia ya kujitolea damu, Juni 14, 2016
Mkuu wa idara ya Damu, Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambaye pia ni Daktari bingwa wa Damu, Dkt. Alex Magesa akiwaeleza waandishi wa habari jinsi damu inavyohitajika sana katika shughuli za tiba. "Kwa sasa mahitaji ya damu kwenye hospitali yetu yamekuwa yakiongezeka kutokana na ongezeko kubwa lawagonjwa, mathalan, tunahitaji damu kati ya lita 100 hadi 130 kwa siku, lakini kiasi ambacho tumekuwa tukipata ni lita 60 hadi 100 tu kwa siku, hapoutaona kuna upungufu wa lita kati ya 20 hadi 40". Alisema Dkt. Alex.
Baadhi ya madaktari wa Kichina waliokoMuhimbili kwa sasa
Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
Balozi wa China akipata chai huku akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, MNH, Bw. Makwaia Makani na maafisa wenginewa juu wa hospitali hiyo
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya Umma, cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Bw. Aminieli Aligaisha (Kushoto), akitazama jambo fulani na maafisa hawa kutoka Ubalozi wa China, XU Jingchun na Bw. Song(kulia)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.