Na Zainab Nyamka, Dar
KLABU ya Yanga SC imetaja viingilio vya mchezo wa kimataifa wa kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe, utakaochezwa siku ya Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam saa kumi jioni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo, yaliyopo Jangwani, jijini Dar es Salaam mchana wa leo, Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema viingilio hivyo ni Sh. 7000 kwa majukwaa ya mzunguko, machungwa na bluu huku VIP B&C 25,000 na Sh. 30,000 kwa VIP A.
Muro amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumatatu katika maeneo mbalimbali na kuwataka mashabiki kuja kwa wingi kuishangilia timu yao ambapo wanatakiwa kuhakikisha hawapotezi mchezo huo tena wakiwa uwanja wa nyumbani.
Huo utakuwa ni mchezo wa pili wa Kundi A kwa Yanga, baada ya Jumapili kufungwa 1-0 na wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, huku TP Mazembe nao wakifanikiwa kushinda mchezo wao wa kwanza dhidi ya Madeama ya Ghana.
Mtaribu wa Matawi na Mkuu wa masoko wa Yanga, Omary Kaaya amesema kuwa anawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na zaidi wawe watulivu kwani wanachotakiwa kukifanya ni kuishangilia timu yao mwanzo hadi mwisho.
WAKATI HUO HUO,
Wachezaji wa Yanga wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam, kwa mafungu jioni ya leo kutokana na kukosa ndege ya pamoja, ambapo imeelezwa waliofanikiwa ni jumla ya wachezaji saba pekee huku wengine wakitazamiwa kuwasili muda wowote usiku huu.
WAKATI HUO HUO,
Wachezaji wa Yanga wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam, kwa mafungu jioni ya leo kutokana na kukosa ndege ya pamoja, ambapo imeelezwa waliofanikiwa ni jumla ya wachezaji saba pekee huku wengine wakitazamiwa kuwasili muda wowote usiku huu.
No comments:
Post a Comment