Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi kutoka
nchini Zambia John Sikazwe akisaidiwa na Jersom Emiliano Dos Santos kutoka
Angola pamoja na Berhe O' Michael wa Eritrea huku mwamuzi wa akiba akiwa
Wellington Kaoma kutoka Zambia.
Kamisaa wa mchezo huo atakuwa ni Celestine
Ntagungira kutoka Rwanda.
Yanga itavaana na Mazembe huku ikiwa imetoka kupoteza mchezo
wake wa awali dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria kwa kukubali
kichapo cha goli 1-0.
Katika mchezo huo Yanga walitengeneza nafasi kadhaa lakini
walishindwa kuzitumia ipasavyo na kupelekea kupoteza mchezo huo wa
awali.
Aidha ushindi huo unaifanya MO Bejaia kushika nafasi ya pili katika kundi A
nyumba ya Mabingwa wa Afrika TP Mazembe huku Yanga ikishika nafasi ya tatu.
Mchezo unaoikutanisha miamba hiyo ya soka unatarajiwa kuwa
mgumu kutokana na Yanga kuhitaji ushindi katika mchezo wake wa kwanza nyumbani
katika mashindano hayo. Kwa sasa Yanga wamerejea kambini nchini Uturuki kwa
ajili ya maandalizi dhidi ya mazembe huku wakitarajiwa kutua nchini siku mbili
kabla ya mchezo wao.
No comments:
Post a Comment