TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U-17), Serengeti
boys imesema ipo fiti kuwavaa Washelisheli katika mchezo wao wa kimataifa unaotarajiwa kuchezwa Juni
26 huku waamuzi wakitokea nchini
Ethiopia.
Mwamuzi wa kati katika mchezo huo ni Belay Tadesse Asserese
atakayesaidiwa na Tigle Belachew, Kinfe Yilma Kinfe, Lemma Nigussie atakuwa
mwamuzi wa mezahi huku kamisaa wa mchezo huo Kalombo Bester akitokea nchini
Malawi.
Akizungumzia maandalizi hayo kocha mkuu wa timu hiyo Bakari
Shime, amesema kuwa kitu kikubwa katika mchezo huo ni ushindi si
vinginevyo. Tangu timu yake iingie kambini Juni 14 mwaka huu
wamefanya kazi kubwa ya kuwaandaa vijana kisaikolojia ili kuhakikisha
wanashinda mchezo huo.
"Kwa ushirikiano
mkubwa wa bechi la ufundi la timu hii tumeweza kushirikiana vvema na mwalimu
Kim Polsen, vijana wameonesha morali kubwa ya mchezo huo, maandalizi
tuliyoyafanya tangu tulipoanza kambi hadi kuelekea mchezo wetu dhidi ya
Shelisheli matumaini makubwa yapo katika ushindi kwani hatuwazi kupoteza kwa
namna yoyote ile ", alisema Shime.
Aidha Shime amewataka watanzania
kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa vijana hamasa ya kufanya vizuri.
No comments:
Post a Comment