Na Zainab Nyamka, Dar
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga stars)
kinatarajia kuwekwa hadharani mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya kuianza kambi ya siku 10 kabla ya mchezo wao
wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda huku wakipatiwa
mwalimu maalumu kutoka nchini Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea katika mashindano ya fainali za mataifa ya Afrika kwa upande wa
wanawake.
Rwanda ilituma mwaliko huo kutokana na kiwango kizuri
walichokionesha Twiga katika michezo yake mbalimbali ya kimataifa waliyoicheza.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
Alfredy Lucas, alisema mchezo huo ni mwaliko maalumu kutoka kwa Rais wa Rwanda
Paul Kagame kwa ajili ya kuwapa burudani viongozi watakaohudhuria mkutano mkuu
wa nchi za Afrika AU. Mkutano huo unatarajiwa kuanza Julai 14 hadi 16 mwaka
huu hivyo anataka kuonesha viongozi hao kuwa hata wanawake wanaweza.
Amesema, kwa kipindi kirefu wanawake wamechukuliwa kama
viumbe dhaifu hivyo mchezo huo utasaidia kuondoa fikra hizo.
"Tunatumai kuwa Twiga wataonesha kiwango kizuri katika
mchezo huo na kuleta ushindani mkubwa ili kudhihirisha kuwa si wanaume tu ndio
wanaoweza kusakata kabumbu bali hata wanawake wanauwezo mkubwa katika mchezo
huo", alisema Alfred.
No comments:
Post a Comment