Na Zainab Nyamka, Dar
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi, ametuma salamu za pongezi kwa Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka nchini (FAT sasa TFF), Michael Wambura kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM).
Wambura ambaye ni Kamishna wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa FAM baada ya kupata jumla ya kura 26 kati ya 27 zilizopigwa.
Katika uchaguzi huo Wambura hakuwa na mpinzani katika nafasi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Musoma Mjini.
Mbali na kumpongeza Wambura Malinzi pia ametuma salamu zake za pongezi kwa Mwenyekiti mypa wa Chama cha mpira wa Miguu mkoani Mtwara, Bw. Kambi
Akizungumza kwa niaba ya Malinzi, Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kuwa Malinzi anamatumaini ya kuwa viongiozi hao watazitumikia vvema nafasi zao.
Alisema, kwa kipindi kirefu soka limeshindwa kuongozwa vizuri katika ngazi za mikoa hivyo kupitia wao mambo huenda yakabadilika.
"Ni matumaini ya Rais kuwa viongozi hao watasimamia vvema michezo na kukuza soka la sehemu walizopo ili kuhakikisha zinakuwa mfano wa kuigwa", alisema Alfred.
No comments:
Post a Comment