Na Daudi
Manongi,MAELEZO.
Mkurugenzi Mkuu
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Bw.Godlove Mbwaji amehaidi kufanya kikao
na uongozi wa waendesha bodaboda wa mkoa wa mbeya ili kuzungumzia suala la waendesha pikipiki hao kuvamia
hospitali hiyo wakiwa katika kundi kubwa wakati wanapofiwa na dereva mwenzao na kusababisha
usumbufu kwa wagonjwa na wakazi wa mbeya.
Mkurugenzi uyo ametoa
rai kwa waendesha bodaboda hao kuwa na nidhamu wanapoingia katika hospitali
hiyo kwani inatumiwa na wakazi wote wa Jiji la Mbeya na husababisha hatari kwa
wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura hospitali hapo kwani huziba barabara yote.
Aidha ameuomba
uongozi wa waendesha bodaboda hao kuchagua watu wachache wanapokuja kuchukua
mwili wa mwenzao kwani itasaidia kupunguza kelele za honi na vyombo vyenyewe
kwani pia kuna majirani wanaokaa katika eneo hilo wanatumia barabara hizo na
hivyo kuepusha ajali.
Pia Bw.Mbwaji ametoa
ushauri kwa uongozi wa waendesha bodaboda hao kuacha vitendo vya uvunjifu wa
sheria na wafuate Sheria,Kanuni na taratibu za Barabarani pale mmoja wapo anapokamatwa au kugongwa kwa
kutojicjhukulia sheria mkononi kumpiga aliyemgonga au kuwafanyia fujo polisi
kwa kumvamia muhusika wakiwa katika makundi makubwa na hivyo kuhatarisha
usalama wa Raia.
Aidha baadhi ya
madereva bodaboda wa mkoa huo wamesema kuwa wamekuwa wakishinikizwa na viongozi
wa matawi yao kwa madai kuwa atakayekataa kwenda kwenye maandamano atatozwa
faini ya sh.50000, hata kama amebeba abiria ulazimishwa kumshusha.
No comments:
Post a Comment