Msemaji wa Yanga, Jerry Muro, akizungumzana waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,leo kuhusu mashabiki wa Simba waliojitokeza kuwaunga mkono watani waowa jadi Yanga katika kuishangilia Yanga kwenye mchezo wa kesho dhidi ya TPMazembe.
Na Zainab Nyamka, Dar
BALOZI wa Amani wa Simba, Risasi Mwaulanga amewataka Wanachama wa Simba na wapenzi na mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kuishangilia na kuisapoti timu ya Yanga katika mchezo wake wa kimataifa waKombe la Shirikisho Afrika CAF dhidi ya TPMazembe unaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Balozi huyo aliyeongozana na baadhi ya wanachama wa Simba kutoka Wilaya ya Temeke wamesema kuwa uzalendo na Utaifa unatakiwa kuwekwa mbele na wao kama wapenda soka basi hakuna budi kuweza kuishangilia Yanga kwani kama wakifanya vizuri nchi itajitangaza zaidi kisoka.
Aidha alisema kuwa, kuna wanachama wengi wa Simba ambao watajitokeza kwa wingi kuweza kuisapoti Yanga katika mchezo huo pia wanaamini kuwa kama watafanya vizuri na kuchukua kombe basi wataongeza timu katika michuano ya kimataifa. "Tunapocheza kwenye mechi za ligi tunakuwa na ushindani ila wakati mtani wetu anacheza mechi za kimataifa ni lazima tuonyeshe uzalendo na kuishangilia kwa juhudi zetu zote ili iweze kufanya vizuri,".
Naye Mkuu wa Kitengo wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amesema kuwa anafurahishwa sana na hatua ya wanachama hao kujitokeza na kuisapoti timu yao hasa katika kipindi hiki cha michuano ya kimataifa na zaidi mafanikio ya Yanga yataitangaza zaidi nchi.
"Tunawashukuru sana wanachama wa Simba kwa kujitikeza kuja kutuunga mkono timu yetu kwenye michuano ya kimataifa na sisi tunaungana nao pia tunapenda kuwaomba radhi Wanachama wa Simba na uongozi kwa ujumla kwa kitendo cha wanachama wetu miaka ya nyuma kwa kuwashangilia TP Mazembe na kitendo hicho hakitajirudia tena,"alisema Muro.
Amewaomba wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi na wakivaa jezi zao pamoja na timu zingine kuja kuisapoti Yanga na ambapo pia alimshukuru aliyekuwa Rais Wa Simba Ismail Aden Rage kwa hatua aliyoionesha kwa kuisapoti katika kipindi chote.
No comments:
Post a Comment