Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati) akiongea na Wakuu wa
Vitengo vya Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani) ambao aliwataka kutengeneza
mikakati madhubuti itakayoimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma. Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa na kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Jamal Zubeir.
Wakuu wa Vitengo vya
Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wa kikao cha pamoja ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho
ya Wiki ya utumishi wa umma.
Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini Kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bi.
Prisca Ulomi akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mh. Nape Nnauye kwa niaba na Maafisa Mawasiliano wakati wa kikao cha
pamoja kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini Leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
No comments:
Post a Comment