Habari za Punde

*KOZI YA UKOCHA MWANZA YAAHIRISHWA


Kozi ya ukocha Mwanza Kozi ya ukocha wa mpira wa miguu ngazi ya leseni C iliyokuwa ianze Jumatatu Juni 20, 2016 imesogezwa mbele
Kozi hiyo iliyopangwa kutolewa kwa mtaala wa Shirikisho la Mpira a Miguu Barani Afrika (CAF) na kufundishwa na Mkufunzi wa CAF-Tanzania, Wilfred Kidao, sasa itafanyika kuanzia Agosti 8, 2016 na kufikia kikomo Agosti 22, 2016.
Sababu za kuahirishwa muda ni kuitikia ombi la washiriki waliopo jijini Mwanza ambao ni zaidi ya asilimia 75 walituma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuomba kusogezwa mbele kwa kozi hiyo kwa sababu za kutumikia vema Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
TFF imekubaliana na maombi yao na hivyo linaomba radhi washiriki wanaotoka nje ya Mkoa wa Mwanza kwa mabadilko hayo. Tunaomba washiriki hao kutoka nje ya Mwanza wasisafiri hadi Agosti, 2016.
Kwa washiriki ambao wamelipa michango yao kwa ajili ya kozi hiyo waendelee kusubiri isipokuwa kwa washiriki ambao hawajalipa michango yao walipe sasa na mwisho ni washiriki 40 tu kwani wakitimia idadi hiyo Idara ya Ufundi ya TFF, litafunga milango.
Hadi sasa waliolipa mchango wa Sh 200,000 kwa ajili ya kozi hiyo ni 29 hivyo nafasi zilizobaki ni 11. Kozi hiyo inaratibwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Vedastus Lufano ambaye anapatikana Mwanza kwa simu Na. 0753 372 068

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.