Habari za Punde

*MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akibadilishana mawazo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu, Mhe. Antony Mavunde akijibu maswali ya Wabunge leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Mhe. Almas Maige akiuliza swali Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Wabunge wa CCM Viti (Maalum) kutoka kushoto, Christine Ishengoma, Martha Umbulla na Magreth Sitta wakibadilishana mawazo ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo leo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Halima Bulembo, akiuliza swali Bungeni leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya Bunge hilo. Kulia ni Mbunge wa Busega, Mhe. Raphael Chegeni.
Naibu Spika wa Bunge, Mhe.Dkt. Tulia Ackson akifurahia jambo na Mbunge wa Kibiti, Mhe. Ally Ungando mara baada ya kuahirisha kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma. PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.