Habari za Punde

*YANGA HAKUNA MAJERUHI TUPO GADO: MURO

 Beki wa Yanga, Juma Abdul, akifanyishwa mazoezi na daktari wake leo kufuatia kuwa majeruhi huku ikielezwa kuwa kwa sasa yupo fiti kuwavaa To Mazembe.
**************************
Na Zainab Nyamka, Dar
BENCHI la Ufundi la Kikosi cha Yanga limeweka wazi kuwa hali ya beki wake wa kushoto Oscar Joshua aliyeumia katika mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia anaendelea vizuri na atarejea uwanjani tena kukipiga na TP Mazembe huku beki wa kulia Juma Abdul akiendelea vizuri na anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi mepesi.

Abdul alikosa mechi ya awali baada ya kuwa majeruhi kwa kuumia sehemu ya kifundo cha mguu na kuukosa mchezo wa kwanza na nafasi yake ikichukuliwa na Mbuyi Twite. Hata hivyo kwa sasa anaendelea vizuri na daktari ameweka wazi kuwa anaweza kuanza mazoezi na timu itakaporejea ataungana na wenzake.

Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa Joshua anaendelea vizuri na watakaoukosa mchezo huo ni Beki wa kushoto Mwinyi Haji aliyepata kadi nyekundu pamoja na mshambuliaji Amisi Tambwe mwenye kadi mbili za njano alizozipata kwenye mchezo wa marudiano na Segrada Esperanca ya Angola na wa hatua ya makundi na Mo Bejaia.

"Ni wachezaji wawili tu ndiyo watakaokosa mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao ni Mwinyi anayetumikia kadi nyekundu na Tambwe mwenye kadi mbili za njano, kwahiyo katika mchezo huo Oscar atarejea tena uwanjani na Abdul anaendelea vizuri ameanza mazoezi mepesi mepesi na pindi timu itakaporejea ataungana nao,"amesema Muro.

Kwa sasa Yanga inaendelea na mazoezi katika jiji la Antalya nchini Uturuki ikiwa inajiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe ambao utapigigwa Siku ya Jumanne Juni 28 au jumatano kumi 29 na unatarajiwa kuwa wa ushindani wa hali ya juu hasa baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa awali na wakihitaji matokeo na TP Mazembe wakitaka ushindi ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kuingia nusu fainali.
 Juma Abdul,akiendelea na mazoezi madogo madogo
Juma Abdul,akiendelea na mazoezi madogo madogodo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.