Na Zainab Nyamka, Dar
MSHAMBULIAJI wa Toto Afrika Waziri Junior, ameweka wazi msimamo wake wa kusaka maisha mapya ya soka nje ya timu yake Toto Afrika baada ya kumaliza mkataba wake ambapo hadi sasa Junior ana asilimia hamsini kwa hamsini za kuondoka au kusalia ndani ya timu hiyo.
Junior pia ameweza kuisaidia timu hiyo kusalia ndani ya ligi msimu ujao baada ya kuwa katika hatihati za kushuka daraja huku wakimaliza ligi wakiwa nafasi ya 13 kwa alama 30.
Msimu uliopita mchezaji huyo alikuwa mwiba kwa Wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba ya baada kuwafunga goli la pekee katika dimba la uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa 24 wa raundi ya pili ya Ligi kuu ya Vodacom.
Junior amesema kuwa kwa sasa hawezi kusema kuwa ana asilimia kubwa za kuondoka ndani ya kikosi cha Toto kwani hilo litajulikana baada ya kukamilika kwa usajili, kwani timu kadhaa zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yake msimu ujao ikiwemo timu yake hiyo lakini bado hajafikiria ni wapi atakapokuwa msimu ujao.
"Timu nyingi zimeonesha nia ya kunihitahi huku Toto pia wakionesha kutaka kunibakiza msimu ujao lakini mpaka sasa sijaamua chochote kwani bado mapema ndio kwanza tumetoka mapumziko,
Kwa sasa naendelea kujiweka sawa na mazoezi ili kuhakikisha nakuwa fiti pindi ligi itakapoanza.
No comments:
Post a Comment