Na Zainab Nyamka, Dar
KUTOKANA na mkanganyiko wa uendeshaji wa mchakato wa
uchaguzi katika Klabu ya Stand United ya mjini Shinyanga, Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), limeagiza michakato yote miwili ule ya Juni 26 na 24 ambayo yote inaendeshwa kwa pamoja ndani ya klabu ya Stand United, isimamishwe mara moja kisha kusubiri maelekezo
mengine.
Hilo limekuja baada ya kutokea sintofahamu kwa pande mbili tofauti
kufanya uchaguzi kwa nyakati tofauti
moja ikijiita Kampuni na wengine wakijiita wanachama wa Stand United.
Akizungumza na Ripota wa mtandao huu, Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu hiyo, Muhibu Kanu
kwa niaba ya Stand United Kampuni amesema kuwa wamesitisha uchaguzi huo mpaka
pale watakapopewa angalizo na TFF kwani wao wanafahamu mchakato mzima jinsi
ulivyo ndani ya klabu hiyo pamoja na hao wanaojiita wanachama.
"Tumepokea
barua kutoka TFF ikituambia kuwa tuache mchakato wa uchaguzi na sisi tumetii
kwani tunachofahamu sisi ndiyo wenye haki na mamlaka zaidi tunachosubiri ni
maamuzi yao".
Aidha Kanu alisema kuwa, baadhi ya watu hawaitakii mema klabu hiyo
zaidi wanachotaka ni kuona kila siku inakuwa katika migogoro na isiyokuwa na manufaa na kudhoofisha maendeleo, kitu
ambacho si kizuri na wanachotakiwa ni kuacha uongozi unaotambulika kufanya kazi
yake kwa ufasaha na kuitoa timu katika kiza kinene mahala
ilipo na kuipeleka juu Zaidi.
"Wanachoona ni kuwa timu imepata mdhamini na ametaka
kuleta maendeleo kwenye klabu yetu wanaanza kujitokeza kwa kuanzisha mchakato
wa uchaguzi na wakijiita wanachama wa Stand ilihali kuwa wanafahamu kuwa kwa
sasa tumesajili kama kampuni na wale wanachama wote wa halali tulioanza na timu
tulikaa chini kwenye mkutano mkuu na kukubaliana kwa pamoja,"alisema Kanu.
No comments:
Post a Comment