HABARI zilizotufikia hivi punde Mtandao huu zinasema kuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji, amejiuzulu wadhifa wake wa kuiongoza Yanga na kuamua kukaa pembeni.
Mbali na kujiuzulu huko pia imeelezwa na chanzo cha uuhakika kutoka ndani ya Klabu hiyo, kuwa Mwenyekiti huyo pia ameamua kusitisha lengo lake la kuimiliki Yanga na Nembo yake ili kuiendesha kibiashsra.
''Endapo maamuzi ya Mwenyekiti huyo yatakuwa ni kama zilivyoenea habari katika baadhi ya mitandao basi litakuwa ni pigo kubwa sana kwa wanayanga, waliokwisha jenga imani kubwa kwa Mwenyekiti huyo''. alisema shabiki mmoja wa Yanga.
Aidha imeelezwa kuwa chanzo cha Manji kujitoa Yanga ni pamoja na figisu figisu za baadhi ya viongozi wa Serikali zinazomshutumu na baadhi ya Wananchama wa Yanga wasio kubari mageuzi anayotaka kuyafanya ndani ya Klabu hiyo, ambao wengi wao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara.
Miongoni mwa watu wanaoweza kuwa kichwani mwa Mwenyekiti huyo hadi sasa pia anaweza kuwepo Katibu Baraza la wazee Mzee Akili Mali, aliyesikika hewani jana majira ya jioni akihojiwa na kituo kimoja na cha redio huku akimshutumu Mwenyekiti wake 'eti kuwa amekurupuka' kutaka kuichukua timu yao.
Manji anaonekana kuchoshwa na tabia za baadhi ya watu kumtukana na kumkebehi kwa hatua yake ya kuichukua timu ya Yanga na sasa ameamua kukaa pembeni kulinda heshima yake.
Hata hivyo viongozi wa Secretarieti ya Yanga leo wameonekana kuchanganyikiwa huku baadhi wakiwa wanapigana vikumbo kuingia na kutoka Ofisi za Manji zilizopo Quality plaza.
No comments:
Post a Comment