Habari za Punde

*TAE KWON-DO YATAMBA KENYA, ETHIOPIA

Na Mwandishi Wetu, Dar
TIMU ya Taifa ya mchezo wa Tae Kwon-do ya Tanzania imefanya vizuri katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika Kenya mwishoni mwa wiki na Tanzania nafasi ya tatu kati ya nchi tano zilizoshiriki.
Rais wa Tanzania Tae-Kwon-do Association( TTA,) Kennedy Said alisema jana kuwa baada ya mashindano hayo Tanzania ilishiriki katika mashindano mengine ya Afrika yaliyofanyika Ethiopia na kushika nafasi ya tatu.
Alisema katika mashindano yaliyofanyika Kenya wachezaji waliotia fora ni John Masawe, Max Kailangana, Said Kennedy na Mustapha Yusuph na Hamadi ismail ambao walizawadiwa medali ya shaba.
Kennedy alisema baada ya kumalizika mashindano  hayo Tanzania ilishiriki mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Ethiopia na kushirikisha nchi 12 ambapo ilishika nafasi ya tatu.
Aliwataja wachezaji walioiletea ushindi Tanzania katika mashindano hayo ni John Masawe na Kennedy ambao waliingia fainali ya mashindano hayo.Kennedy alifaulu katika uvunjaji wa vitu vigumu na Masawe alingia katika kucheza mchanganyiko ya vitu mbalimbali.
Rais Kennedy alisema baada ya mashindano hayo ulifanyika mkutano wa uchaguzi wa kuchagua viongozi wa mchezo huo Afrika.Katika uchaguzi huo Rais wa mchezo huo Afrika ni Gatchew Tamrat kuwa Rais wa Afrika Tae-Kwon-do Afrika ATF na Katibu kutoka AFrika Kusini na Mweka Hazina ni Tafita A. Tafita kutoka Madagascar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.