*YANGA, AFRICAN LYON WAKAMILISHA USAJILI KWA TMS.

Na Mwandishi Wetu, Dar
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Nchini TFF, limethibisha kukamilika kwa usajili wa timu 11 zilizokuwa hazijakamilisha usajili wake kwa mfumo wa TMS baada ya kuongezewa muda wa masaa 48 baada ya kufungwa kwa dirisha la awali.
Akizungumza na Mtandao huu, Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa timu zote 11 zimeshakamilisha usajili wake kwa njia ya TMS baada ya kuongezewa muda wa masaa 48 na shirikisho la mpira wa Miguu Duniani FIFA.
Awali dirisha la usajili nchini lilifungwa Agosti 06 huku timu kadhaa ikiwemo Yanga na African Lyon za ligi kuu zikiwa hazijafanya usajili wake n kutakiwa kuandika barua za utetezi ili kuweza kupata fursa ya kufunguliwa tena kwa dirisha la usajili.
Lucas amesem kuwa, baada ya kutum utetezi wao uliwasilishwa FIFA na wakapewa masaa 48 kukamilisha usajili huo huku TFF wakizipiga faini timu za ligi kuu kwa kulipa kiasi cha milioni tatu na timu za ligi daraja la kwanza wakitakiwa kulipa milioni moja.
Kumalizika kwa usajili huo timu kwa sasa zinaweza kuendelea na taratibu za kujiandaa na ligi huku wakisubiri mapingamizi kwa wachezaji waliowasajili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Templateism Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.