Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS NA WATU TISA WAPOTEA NA NDEGE KUSIKOJULIKANA

Ndege ya Jeshi la nchini Malawi, iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Saulos Chilima na wasaidizi wake tisa, imepotea kusiko julikana.
Taarifa za kupotea kwa ndege hiyo zilitolewa na Ofisi ya Rais wa Malawi, muda mchache baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege mji mkuu wa Lilongwe.
Aidha Mamlaka ya usafiri wa Anga ya nchi hiyo ilithibitisha hayo baada ya juhudi za kuisaka ndege hiyo katika rada kugonga ukuta.
Chilima (51) aliondoka mji mkuu wa Lilongwe jana majira ya saa tatu asubuhi akielekea Kaskazini mwa nchi hiyo ambako alikuwa akienda katika shughuli za maziko ya Waziri wa zamani Ralfi Kasambala aliyefariki siku nne zilizopita.
Ikumbukwe kuwa Chilima aliingia madarakani rasmi mwaka 2014 na 2020 kuingia tena madarakani kwa awamu ya pili baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliokuwa na mvutano mkubwa kati ya chama tawala na chama pinzani.
Aidha Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ameahirisha mipango yake ya safari kwenda Bahamas na ameagiza juhudi zote zielekezwe kwenye utafutaji na uokoaji.
Mkasa huu unajiri wiki kadhaa tangu kuanguka kwa ndege ya helikopta iliyoua Rais Ebrahim wa Iran na maafisa wengine tisa akiwemo Waziri wa Mashauri ya Kigeni.
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.