Wananchi waliobeba jeneza la mwili wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi yaliyofanyika Nyumbani kwake Migombani Unguja leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya mapinduzi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika mazishi ya Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi yaliyofanyika Nyumbani kwake Migombani Unguja leo mchana.
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Aboud Jumbe likiwasili nyumbani kwa marehemu Migombani, Zanzibar
Watoto, Ndugu, jamaa na Viongozi mbali mbali wakipokea mwili wa Marehemu Mzee Aboud Jumbe mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Migombani ,Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalum mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ,nyumbani kwa marehemu Migombani Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akishiriki dua maalum kwenye msiba wa Mzee Aboud Jumbe nyumbani kwa marehemu Migombani , Zanzibar wengine pichani ni Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Mwanamema Shein (kushoto) kulia ni mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa
Safari ya kwenda msikitini kuswaliwa
No comments:
Post a Comment