Habari za Punde

*MTANGAZAJI WA CLOUDS TV HUDSON KAMOGA ATEULIWA MKURUGENZI WILAYA YA MBULU

Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga
**********************************
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga, ambaye ameteuliwa mwishoni mwa wiki jana amesema anaamini ni Mungu aliyemuweka kwenye nafasi hiyo ili awatumikie wananchi wa Mbulu kwa wakati huu. 

Akiongea kwenye ibada ya Jumapili hii ndani ya Kanisa la Living Water Center Kawe, wakati alipopewa nafasi na mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi ili asalimia Kanisa Mheshimiwa Kamoga alisema, anakwenda kwenye wilaya yenye changamoto nyingi za kimaendeleo ila anaamini Mungu atamwezesha kuzitatua kwa nafasi yake akishirikina na wananchi pamoja na viongozi wengine kati halimashauri ya Mbulu.

Kamonga alisisitiza kuwa kwa kupata nafasi hii ya Ukurugenzi bado ataendelea na utumishi wake kwa Mungu maana anaamini huo ndio uliomfanya kufikia hatua hiyo,hivyo kuamua kuwa anamtanguliza Mungu kaika kila atakachokuwa anafanya,alisema Kamoga
Pia alitoa shukurani za dhati kwa Mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi pamoja na watumishi wengine kanisani hapo na kusema kuwa kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau na malezi mazuri ya kiroho pamoja na mafindisho ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa Apostle Ndegi na watumishi wengine kanisani hapo, akisema mafundisho hayo yamesababisha kuwa vile alivyo sasa! Mwisho Mtumishi wa Mungu Mtume Onesmo Ndegi na waumini walifanya maombi kwa ajili yake ili Mungu aambatane naye katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo ya Ukurugenzi!.
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake. 
Mkurugenzi mteule wa Wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga akiwa na Baba yake wa Kiroho Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimsiliza kwa makini akielezea uteuzi wake. 
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe akimwombea Hudson Kamogaakiwa amepiga magoti 
Waumini wa Kanisani Living Water Center Kawe wakiwa wamenyoosha mikono kwa Hudson Kamoga kuomba kwa ajili yake 

1 comment:

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.