Wachezaji wa Yanga wakimpongeza mwenzao Haji Mwinyi, baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza. Bao la Ngaya lilifungwa katika dakika ya 19 pia kipindi cha kwanza, ambapo mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Haji Mwinyi akimtoka beki wa Ngaya.
************************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Wawakilishi
Tanzania Bara katika ligi ya mabingwa Afrika, Yanga sasa itacheza na wakilishi
wa Zambia, timu ya Zanaco FC kabla ya kufuzu hatua ya makundi.
Yanga imefikia
hatua hiyo baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Ngaya Club ya Comoro
na kufanikiwa kufuzu hatua hiyo kwa idadi ya mabao ya kufunga 6-2.
Zanaco imefuzu
hatua hiyo baada ya kushinda mabo 1-0 dhidi ya APR ya Rwanda mjini, Kigali
mapema leo. Yanga itaanzia nyumbani Machi 10 kabla ya kusafiri kwenda Lusaka
Machi 17.
Yanga
inahitaji kushinda mechi hiyo ili iweze kufuzu katika hatua ya makundi na
baaaye robo fainali, kabla ya kucheza nusu fainali na fainali.
Ngaya ilianza
mchezo kwa kasi na kutafuta mabao ya kuwawezesha kufuzu katika hatua inayofuata
na kupata bao la kuongoza katika dakika ya 19 kupitia kwa Zamir Mohamed.
Shuti kali la
Zamir lilimbabatiza beki wa Yanga, Vincent Bossou na kumpita kirahisi kipa
wake, Deogratius Munish. Baada ya bao hilo,
Yanga ilikuja juu kwa lengo la kutafuta bao la kusawazisha. kusoma zaidi bofya hapa
Juhudi za
Yanga ziliishia kwa wachezaji wake kupiga nje au kupoga ‘kiduchu’ na kipa wa
Ngaya Said Mmadi kuokoa kirahisi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Wachezaji wa
Yanga walihisi kuwa kuna ‘uchawi’ kwenye lango la Ngaya na kwenda kufukua na
kukuta sarafu (senti tano ya Kitanzania) na kuitupa.
Baada ya kutoa
sentitano hiyo iliyowekwa na kipa wa Ngaya, Yanga ilisawazisha katika dakika ya
43 kupitia kwa Haji Mwinyi aliyepiga shuti kali la mita 35.
Yanga
ilionekana kujiamini zaidi katika mchezo huo na kutengeneza nafasi nyingi za
kufunga, hata hivyo, wachezaji wake, Emmanuel Martin, Juma Mahadi, Simon Msuva na Obrey Chirwa
walipoteza nafasi hizo.
Kocha wa
Yanga, Juma Mwambusi aliwapongeza wachezaji wake kwa kufuzu hatua hiyo na sasa
kufikiria mechi ya Zanaco.
“Tulichotaka
ni kufuzu na tumefanikiwa kufikia hatua hiyo, hivyo wachezaji wanastahili
kupongezwa, tumefanya makosa mengi, hata hivyo muda tunao na tunaahidi
kuyarekebisha katika mechi zijazo,” alisema Mwambusi.
Nahodha wa
Ngaya, Said Hachim aliwapongeza wachezaji wenzake kwa matokeo hayo mazuri kwao.
Hachim alisema hawakutegemea kutoka sare na Yanga baada ya kupoteza mchezo wa
kwanza.
“Tulikuja hapa
kwa lengo moja la kuzuia kufungwa, tulifanya makosa katika mchezo wa kwanza na
kufungwa mabao 5-1, leng letu limetimia na sasa tunafuraha kubwa sana, Yanga ni
timu kubwa sana,” alisema Hachim.
Kaseke akimpongeza Haji.
Kipa wa Ngaya, akiruka kudaka mpira kuokoa hatari langoni kwake.
Msuva akituliza mpora gambani huku kipa wa Ngaya akijiandaa kuokoa
Beki wa Ngaya akiokoa huku Kaseke akijaribu kukaba
Chirwa akijaribu kumroka beki wa Ngaya
Emmanuel Martin akiruka kuwania mpira na beki wa Ngaya
Kipa wa Ngaya akiruka kuokoa hatari
Obrey Chirwa akimtoka beki wa Ngaya
Deus Kaseke akiwania mpira na beki wa Ngaya
Thaban Kamusoko akifanya yake
Kaseke akiwatoka mabeki wa Ngaya


Juma Mahadhi akijaribu kupiga shuti katikati ya mabeki wa Ngaya
Msuva akimtoka beki wa Ngaya
Mahadhi akimfinya beki wa Ngaya


KIKOSI CHA YANGA SC:
Vicent Bossou, Deogratias Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji,
Kelvin Yondani, Justine Zulu, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Deus Kaseke, Obrey
Chirwa na Emmanuel Martin.
BENCHI LA AKIBA:
Ally Mustafa, Hassan Kessy, Said Juma, Vicent Andrew, Nadir
Haroub, Oscar Joshua na Juma Mahadhi.
KIKOSI CHA NGAYA:
Said Hachim, Said Mmadi, Chadhuili Mradabi, Said Anfane, Frank Said, Youssouf Ibrahim, Rakotoarimanana Falinirino, Berthe Alpha, Zamir Mohamed, Mounir Moussa na Said Tohir.
BENCHI LA AKIBA:
Ali Ahamada, Kadafi Said, Chabane Saandi, Abdoul Hafal, Nadjim Nourdine, Adhepeau Denis na Nourdine Said.


















No comments:
Post a Comment