Na
Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea taarifa ya
kina kuhusu chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.
Paul Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media akiwa na walinzi
wenye silaha Machi 17, 2017.
Akipokea
taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas ameishukuru Kamati kwa utulivu wao na
kuifanya kazi hiyo kwa utaalamu na umakini mkubwa huku jamii ikitaka matokeo
kwa haraka.
Aidha
Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili
ya uamuzi na maelekezo.
“Nimeipokea
ripoti na ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa wakubwa zangu wao
ndo wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.
Kamati
aliyoiunda Mhe Waziri ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni Bw.Deodatus Balile
kutoka Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi Nengida Johanes wa
Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Hassan Abbas .

No comments:
Post a Comment