Promota wa ngumi, Jay Msangi (katikati) akiwatambulisha mabondia Francis Cheka 'SMG' (kushoto) na Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' wanaotarajia kupanda jukwaani Desemba 31 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kuwania mkanda wa Mabara wa Shirikisho la ngumi la dunia WBF (World Boxing Federation) uzito wa kg 76 'Super middleweight'. Pambano hilo litakuwa la raundi 12.
*************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
BAADA ya kukimbiana kwa takribani miaka miwli hatimaye sasa wababe wa masumbwi nchini, Dula Mbabe na Francis Cheka kukutana uso kwa uso Desemba 31 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, kuoneshana umwamba katika pambano la raundi 12 uzito wa 'Super middleweight'.
Mabondia hao wamekuwa wakitambia na kwa muda mrefu huku wakipishana ulingoni kila mmoja anapomhitaji mwenzake jambo ambao lilizidisha hamasa kubwa katika mchezo huo huku mashabiki wakiwa na hamu kubwa ya kushuhudia wababe hao pindi watakapofikia muafaka wa kuchapana ulingoni.
Katika kukata kiu za mashabiki wa mchezo huo Promota Jay Msani ameamua kuwakutanisha wakali hao na kuandaa Bongo Daby ya ngumi ambayo kwa hakika itakuwa ni historia kabla na baada ya wakali hao kupanda ulingoni na kupatikana mbabe atakayetangazwa.
No comments:
Post a Comment