Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amefungua mkutano wa pili wa Biashara, Ujasiriamali na Maonyesho wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
Katika mkutano huo ambao unazikutanisha sekta Serikali na Sekta binafsi kutoka nchi wanachama, Makamu wa Rais alisisititiza kuwa pamoja na kuelekea kwenye kujenga Afrika Mashariki ya Viwanda ni muhimu viwanda hivi vitumie malighafi zinazozaliwa ndani ya Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais alisema kujenga uchumi wa viwanda uendani na maboresho ya sera ya viwanda ili itoe uwanja mpana wa kuajiri vijana wengi zaidi.
Makamu wa Rais alihimiza kuwa Viwanda vitakavyojengwa viende sambamba na kilimo kwani kwa pamoja ndipo tunaweza ona mafanikio na ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa Ujumla.

Makamu wa Rais alimalizia kwa kusema kuwa Serikali na Sekta binafsi zinawajibu kushirikiana katika kuandaa mazingira mazuri ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.