Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (wapili kulia),akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima (watatu
kulia) na viongozi wengine, baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba zinazooenekana
pichani za askari polisi na familia zao ulioko
kata ya Mukonde, Mkoani Mara, kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe. Nyumba hizo ziko
katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa
askari hao.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akiongozana
na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Musoma,
Dk. Vicent Naano, kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata
ya Mukonde, Mkoani Mara, Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili
ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari.
Familia
za askari wanaotarajiwa kuhamia katika nyumba mpya zilizopo katika eneo la
Mukonde, wakimsikiliza Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni, wakati alipotembelea kuona maendeleo ya mradi huo ikiwa ni ziara yake
ya kikazi mkoani Mara. Nyumba
hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za
makazi kwa askari.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry Mwaibambe, baada ya kukagua nyumba za askari polisi na familia zao zilizopo kata ya Mukonde, Mkoani Mara,wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mara ,Adam Malima (aliyevaa miwani) na Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dk. Vicent Naano.Nyumba hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika ili ziweze kumaliza changamoto za makazi kwa askari. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment