IMEFAHAMIKA kuwa sasa ni rasmi kuwa Nahodha wa Taifa Stars ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta, ataukosa mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Benin unatajia kuchezwa Novemba 12, mwaka huu kutokana na majeraha ya goti.
Taarifa kutoka kwa matatibu wa Genk ya Ubelgiji, zinasema Samatta anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo ambao utamchukua wiki nne hadi kurejea uwanjani kucheza.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amepokea taarifa hiyo na kusema haijawa bahati kwa Stars, lakini atapanga kikosi chake vema kwa wachezaji atakaokuwanao huko Benin akiwamo Abdi Banda na Farid Mussa pamja na vijana wawili wa Serengeti Boys.
Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa, Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.
No comments:
Post a Comment