Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu), akikagua
gwaride la heshima wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya
Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu) na Meja Jenerali Simon Mumwi (Mstaafu) (kulia aliyesimama kwenye gari), wakisukumwa kwenye gari inayotembea mwendo wa taratibu kuashiria kumalizika kwa utumishi wao katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakati wa hafla ya kuwaaga, iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu) akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Venance Mabeyo, baada ya kumaliza utumishi katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa jeshi hilo, iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Gwaride la Heshima likipita mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu), wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira (Mstaafu) na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dk. Florens Turuka(kulia), wakizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyofanyika leo katika Kambi ya Twalipo iliyopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Ambapo Meja Jenerali Rwegasira (Mstaafu), aliagwa baada ya kumaliza utumishi wake katika jeshi hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment