Habari za Punde

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA ATEMBELEA OFISI ZA TANROADS JIJINI DAR ES SALAAM

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (kushoto), wakati alipotembelewa ofisini kwake, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bw. Boniface Myalla.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (kulia), akimuonesha ramani ya mtandao wa barabara hapa nchini Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, wakati alipotembelea ofisi za wakala huo kujionea utendaji kazi na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakati alipowatembelea kujionea utendaji kazi wao na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya watendaji wa Wakala wa wa Barabara nchini (TANROADS), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa (hayupo pichani), katika kikao kazi wakati alipowatembelea kujionea utendaji kazi wao na kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.