Habari za Punde

SAMATTA AFANYIWA UPASUAJI

Ni taarifa njema kwa watanzania wote hususan wadau wa soka kwamba, nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta upasuaji wake wa goti umefanyika na kumalizika salama.
Samatta aliumia goti November 4, 2017 wakati akiitumikia klabu ya ya KRC Genk ya Ubelgiji na kushindwa kuendelea na mechi dhidi ya Lokeren mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa wa instagram (samagoal77) ameandika ujumbe unaothibisha kwamba upasuaji umefanyika na kumalizika salama.
“Napenda kuwajulisha kuwa, upasuaji wangu umeenda vizuri. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, timu ya madaktari pamoja na mashabiki wangu.”
“Nimepokea meseji nyingi sana kutoka sehemu tofauti duniani na napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa meseji na Dua zenu.”
Baada ya kufanyiwa vipimo, madaktari walimwambia Samatta atakaa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita kabla ya kuanza kucheza tena.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.