Katika kuhakikisha kuwa wanaisaidia Jamii inayowazunguka shirika lisilo la kiserikali la The Foundation Foundation for civil Society limejipanga kuwasaidia watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wanaopatikana katika Taasisi ya mifupa MOI jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa shirika hilo kuadhimisha siku yao maarufu ya “GIVING TUESDAY” ambayo hutumia siku hiyo kuisaidia jamii.
Akieleza mikakati ya kuadhimisha siku hiyo kwa mwaka huu mwakilishi kutoka shirika hilo Ndugu Karin Rupia amesema kuwa baada ya kuona changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wanaohudumiwa katika taasisi hiyo wameamua kuitumia siku hiyo kuwasaidia watoto hao huku akiwataka watanzania kuwaunga mkono katika kutekeleza Jukumu hilo.
Mwakilishi huyo amesema kuwa shughuli hiyo itafanyika kwa siku mbili ambapo siku ya kwanza itakuwa tarehe 25 Novemba ambapo wataitumia kuchangia damu kwa ajili ya watoto hao wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi ,zoezi ambalo litafanyika ndani ya taasisi hiyo ya Mifupa MOI kuanzia saa tatu asubuhi hadi majira ya mchana.
Katika zoezi la pili litafanyika tarehe 28 Novemba ambayo ndiyo siku maalum ya Jumanne ya kutoa “Giving Tuesday” ambapo katika siku hiyo shirika limejipanga kusaidia watoto katika kuwapatia mahitaji mbalimbali ambapo shughuli kubwa itakuwa ni kuwasaidia watoto kupata upasuaji ambapo amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa wanasaidia watoto mia moja kupata huduma hiyo ya upasuaji.pamoja na kuwadaia vifaa mbalimbali vitakavyosaidia katika kwa watoto hao ambapo watanzania wametakiwa kujitolea kuchangia kwa kasi ili kusaidia shirika hilo kufikia malengo hayo.
Ili kushiriki katika zoezi hilo la kuchangia damu kwa ajili ya ,kuwa unaweza kupiga simu namba 0762767237.
Video ikifafanua kuhusu siku hiyo ya Jumanne ya kutoa “Giving Tuesday”
No comments:
Post a Comment