Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akitoa wito kwa
watanazania kujitokeza kwa wingi uwanja
wa uhuru tarehe 25/11/2017 kushangilia pambano la bondia Ibrahim Class
(kushoto) wanchini akitetea ubingwa wa
dunia uzito wa kati na bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini leo jijini Dar es
Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym
Kawe. yake ya mazoezi .
Bondia Ibrahim Class (kulia) akifanya mazoezi na Mwalimu Msaidizi Bw.Kelvin Magembe (kushoto) kuonyesha uwezo wake mbele ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia)alipomtembelea kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano litakalofanyika kati yake na Bondia Koos Sibiya wa Afrika Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017 Uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
Bondia Ibrahim Class (kulia) akimkabidhi zawadi ya tisheti yenye jina lake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake kwa pambano la tarehe 25/11/2017 katika uwanja wa uhuru na bodia wa Afrika ya Kusini kutetea ubingwa wa dunia uzito wa kati leo jijini Dar es Salaam.
*********************************
Na Anitha Jonas WHUSM, Dar
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi
kumshangilia bondia Ibrahim Class katika pambano lake la kutetea ubingwa wa
dunia uzito wa kati na bondia kutoka Afrika ya Kusini Koos
Sibiya.
Mheshimiwa Mwakyembe
ametoa wito huo jana jijini Dar es
Salaam alipomtembelea bondia huyo kambini Joe Gym Kawe kujionea maandalizi yake
bondia kwa pambano litakalofanyika
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam tarehe 25/11/2017.
“Bondia huyo anauwezo
mkubwa na amekwisha kushinda mara mbili kwa Afrika na kwa mkanda huu wa
kugombea ubingwa wa dunia nimeona ni vyema akapigania hapa nchini ili
watanzania waweze kuona uwezo wake na pamoja na kumongezea ari ya kupambana kwa
ajili ya watanzania walikuja kumuunga mkono,”alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Mhe.Mwakyembe
alisema atasimamia mchezo wa ngumi na kuhakikisha
unarudisha heshima yake kama ilivyokuwa zamani kwa kuhakikisha anadhibiti
wapiganaji wanaokwenda kwenye mapambano na kununuliwa huku wakililetea sifa
mbaya taifa ya kutumika kupandisha watu madaraja.
Kwa upande wa Bondia
Ibrahim Class wa nchini aliwahakikishia watanzania kupambana kwa nguvu zote
kuhakikisha anauchukua ubingwa huo na mkanda huo kubaki nchini huku akiwataka
watanzania kuja kujionea wenyewe namna atakavyopambana na kuonyesha uwezo wake.
“ Nataka kuwatoa hofu
watanzania kuwa waje kujionea wenyewe
jinsi gani nitakavyo mpiga huyo mwafrika kusini na kuchukua mkanda nimejiandaa
vizuri na mazoezi ninayofanya niyakiwango cha juu,”alisema bondia Class.
Pamoja na hayo nae Rais
wa TPBC Bw.Chaurembo Palasea aliongeza kuwa mchezo wa ngumi umekuwa na
changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa ulingo kwa ajili ya kufanyia mazoezi kwani
hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa sekta ya mchezo wa ngumi.
Halikadhalika Waziri
Mwakyembe amesema kuwa serikali
itaanzisha bodi itakayosimamia sekta ya ngumi kwa lengo la kuondoa kukosekana
kwa dira ya usimamizi wa sekta ya ngumi nchini.
No comments:
Post a Comment