Habari za Punde

WORLD GREAT SAFARI TOUR 2017/2018 KUTANGAZA UTALII WA AFRIKA MASHARIKI

Taasisi ya Africa Tourism Promotion Centre, yenye makao makuu yake mkoani Pwani Tanzania, kupitia tamasha la kimataifa la World Great Safari Tour , itazindua pango kakati na kapeni kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa nchi za Afrika mashariki na kati kitaifa na kiataifa.
Huu ni mpango na mkakati mahususi, ambao tumeuandaa kwa lengo la kukuza pato litokanalo na utalii miongoni mwa nchi za Afrika mashariki, kwa kuvutia idadi kubwa zaidi ya watalii, kuongeza pato litokanalo na utalii, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje katika sekta ya utaliii, kwa kuvutia watalii wengi zaidi,kuongeza siku za watalii kukaa katika vivutio husika, lakini pia kuondoa ,utegemezi wa watalii wa nje pekee ,kwa kuhamasisha utalii wa ndani na utalii wa kitaaduni,sanaa,utalii wa michezo na burudani.
Kupitia World Great Safari Tour, nchi husika zitapata fulsa ya kutangaza vivutio vyake vya utalii kitaifa na kimataifa, hivyo kuvutia watalii wengi zaidi wa ndani na nje,lakini pia kutangaza zaidi fulsa za uwekezaji wa kitalii zilizopo katika nchi husika ,hivyo kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
World Great Safari Tour– East Africa Tourism Promotion, itahusisha matukio na matamasha makubwa ya kitalii, michezo,burudani,Utamaduni,sanaa na mihadhara na mijadala ya kitaifa na kimataifa ya Utalii na Wanyamapori, Utalii na mazingira, Utalii na Umasikini, pia Utalii na Huduma za Kijamii.
Matukio hayo ni pamoja na fainali za kitaifa za Miss Tourism University World 2017/18,na matamasha ya kitaifa ya National Parks Marathon, Ant Poaching/Wildlife Marathon, National Tourism Awards, National Great Safari Tour ( katika nchi zote husika, na kuhitimishwa na Fainali za Dunia za Miss Tourism University World -2018/19, World Tourism Awards 2018/19, Ant Poaching/Wildlife International Marathon, National Parks International Marathon, na World Great Safari Tour zitafanyiaka Afrika mashariki katika nchi itakayo teuliwa. Nchi hizo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo (DRC), Ethiopia na Sudani.
Mkakati na kampeni hiyo inajulikana kwa jina la WORLD GREAT SAFARI TOUR & TOURISM PROMOTION. Iepangwa kuzinduliwa wezi Disemba 2017,katika nchi na tarehe itakayotangazwa katika press conference itakayo fanyika wishoni wa wezi huu.
Africa Touris Prootion Centre ni taasisi tanzu ya Miss Tourism Tanzania Organization (Miss Tourism Tanzania Beauty Pageant Limited), abao pia ndio wenye dhia ya kikoo ya kuandaa na kuendesha mashindano yenye afanikio kuliko engine yote nchini na afrika ashariki ya Miss Tourism Tanzania Pageant, ambayo taratibu za kuanza kuyaendesha kwa mfumo na utaratibu mpya ziko mbioni kukailihwa,ili yaweze kuanza tena wakani 2018. 

Mr. Gideon Erasto Chipungahelo
MWENYEKITI MTENDAJI
Africa Tourism Promotion Centre
0626 447 180, 0711 356 978, 0756 220 978

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.