Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua
ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha
star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) pamoja na
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) wakifuatilia yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s
TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana
katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi JTV Bw. Sanctus Mtsimbe . KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mkurugenzi Jason’s TV Bw. Sanctus Mtsimbe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli
Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini
Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mtendaji
Bodi ya Filamu Bw. Benson Mkenda
akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua
ikionyesha filamu mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha
star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara
ya Sanaa Bibi. Joyce Hagu akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Chaneli Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu
mpya za kitanzania na inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli
namba 126 jana Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu, Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akibonyeza rimoti kuzindua Chaneli
ya Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe
Rais Mstaafu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiangalia Chaneli ya Jason’s TV (JTV)
baada ya kuizindua jana Jijini Dar es Salaam. JTV itakua ikionyesha filamu mpya
za kitanzania na inapatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba
126.
Rais Mstaafu, Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(waliokaa katikati)
katika picha ya pamoja na wadau wa sekta
ya filamu baada ya kuzindua Chaneli ya
Jason’s TV (JTV) itakayokua ikionyesha filamu mpya za kitanzania na
inayopatikana katika king’amuzi cha star times chaneli namba 126 jana Jijini Dar
es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe. Picha
na:
Genofeva Matemu - WHUSM
******************************************************
Na: Genofeva Matemu –
WHUSM
WADAU mbalimbali ndani
na nje ya nchi wametakiwa kujitokeza na kuwekeza katika vifaa vya kisaa vya
kurekodia filamu ili sekta ya filamu nchini Tanzania iweze kuendelea zaidi na
kuvuka mipaka kwa kuwa na ubora wa kuweza kushindana na filamu za nchi
nyingine.
Rai hiyo imetolewa na Rais
Mstaafu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokua
akizindua chaneli mpya ya Jason’s Televisheni itakayokuwa ikionyesha filamu
mpya za kitanzania inayopatikanakatika king’amuzi cha Star times chaneli namba
126 jana Jijini Dar es Salaam.
“Wadau wa tasnia ya
filamu nchini hasa waandaaji wa filamu mnapaswa kuangalia namna ya kupata wadau
watakaosaidia kuwekeza vifaa vya kisasa vya kurekodia na kwa upande wangu
nitajaribu kuwakutanisha na wadau wenye uwezo wa kuwekeza ili muangalie namna
ya kuzungumza nao na kuwekeza vifaa vitakavyowawezesha kuandaa filamu zenye
ubora na kukidhi hadhi ya kushindana kimataifa” amesema Mhe. Kikwete.
Aidha Mhe. Kikwete
amesema kuwa kuwepo kwa chaneli ya JTV itakayokua ikirusha filamu mpya za
kitanzania ni jambo muhimu sana katika historia ya tasnia ya filamu hapa nchini
hivyo uzinduzi wa chaneli ya JTV unafungua ukurasa mpya katika maendeleo ya
tasnia ya filamu ambayo imekua ikikua kwa kasi.
Mhe. Kikwete amesema
kuwa kufanikiwa kwa chaneli ya JTV
kutapunguza machungu mengi ya watayarishaji wa filamu kwa kutatua
changamoto ya kutokuwa na soko la uhakika na kuleta nuru ya matumaini kwa wasanii
kwa kupata malipo yanayostahili kwa
vipaji vyao, jasho lao pamoja na gharama wanayoingia katika kutengeneza filamu.
Kwa upande wake Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa
uanzishwaji wa chaneli ya JTV ni moja ya mikakati kadhaa ya kuboresha
usambazaji wenye tija wa filamu mpya za kitanzania hivyo kuwataka watayarishaji
wa filamu kuthamini mandhari za filamu zetu kwani filamu iliyokosa hata dakika
moja kuonyesha vivutio vya utalii tulivyonavyo inakosa sifa ya ubora.
Awali Mhe. Mwakyembe
amesema kuwa Tanzania itabaki kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ambayo ni
lugha ya 10 kuzungumzwa na watu wengi duniani kati ya lugha 6000 hivyo ni
matarajio ya wizara baada ya muda mfupi mtu akisikia ala za nyimbo za Kiswahili
katika filamu zetu kama vile Mdumange, Sindimba nk. ajue anaangalia filamu ya
kitanzania.
Naye Kaimu Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bw. Benson
Mkenda amesema kuwa bodi ya filamu ipo tayari kushirikiana na wadau wote katika
tasnia ya filamu wenye nia ya kukuza na kuendeleza tasnia kama ilivyo kwa
Jason’s TV ambao lengo lao mahususi limelenga kuendeleza sekta ya filamu hasa
katika eneo la usambazaji ili kuweza kuitoa sekta hii mahali ilipo na
kuifikisha katika viwango vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment