Msaidizi wa Rais Kanali Msafiri Mkeremy akimkabidhi Imamu wa Msikiti wa Noor kijijini Mkange, Miono, Wilaya ya Chalinze mkoa wa Pwani Sheikh Khamis Nassor wakati alipowasilisha msaada wa zulia la kuswalia msikitini hapo akiwa kaongozana na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Jaffary Haniu (nyuma ya Imamu) leo.
***************************************************************
Waumini
wa dini ya Kiislam wa Msikiti wa Noor uliopo katika Kijiji cha Mkange, Miono, Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani ,wamemshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa
msaada wa zulia la kuswalia na fedha taslim Shilingi milioni Mbili.
Zulia
pamoja na fedha hizo zimekabidhiwa na Msaidizi wa Rais Kanali Mbaraka Mkeremy
kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa Imamu wa Msikiti huo Alhaji
Sheikh Khamis Nassor wa Msikiti Noor uliopo katika kijiji cha Mkange, Wilaya ya
Chalinze mkoa wa Pwani.
Mara
baada ya kukabidhi Zulia na fedha hizo, Kanal Mkeremy kwa niaba ya Rais
Magufuli amewataka waumini wa Msikiti huo kutumia msaada huo kwa lengo
lililokusudiwa.
Akiungumza
mara baada ya kukabidhiwa Msaada huo, Sheikh Nassor amesema kwa niaba ya
waumini wa Msikiti huo wanamshukuru Mhe. Rais kwa kuitikia ombil lao la kupata
zulia, na kwamba kwa kutimiza ahadi yake
hiyo Mhe. Rais amedhihirisha kuwa yeye ni mtu wa watu asiyebagua dini wala
kabila katika kusaidia jamii ya kitanzania.
Sheikh
Nassor amesema waumini wa msikiti huo wanamuombea na wataendelea kumuombea Mheshimiwa Rais na kuwataka
watanzania wote nchini kuungana nao kumuombea Rais bila kujali itikadi za
kisiasa ama imani za kidini kwani anayoyafanya Rais kwa wananchi wa Tanzania ni
kwa manufaa ya wananchi wote.
Jaffar
Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Pwani
17
Novemba 2017.
No comments:
Post a Comment