Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki
Ulisubisya akipokea vifaa vya kufundishia kutoka kwa Balozi wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Dr Detlef Wachter
katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani inayoazimishwa kila Novemba
Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani, ambapo shirika la GIZ kutoka Ujerumani lillikabidhi vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dtk. Wedson Sichalwe akiwasilisha taarifa fupi mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Viongozi na waandishi wa habari(hawapo kwenye picha) katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani.
Meneja mipango wa Shirika la Giz kutoka Ujerumani Dkt. Susanne Grimm akielezea baadhi ya mafanikio na mipango ya Shirika hilo wakati wakitoa msaada wa vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.
Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dr Detlef Wachter akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi na waandishi wa habari wakati wa utoaji msaada uliofanywa na shirika la Giz katika Taasisi ya Saratani Ocean road jijini Dar es salaam, mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akimpa mkono wa shukurani Balozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dr Detlef Wachter baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akifungua mkutano katika maazimisho ya siku ya mtoto njiti duniani, ambapo shirika la GIZ kutoka Ujerumani lillikabidhi vifaa vya kufundishia watoa huduma jinsi ya kuwasaidia watoto njiti.
********************************************
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imepokea msaada wa
vifaa vya kufundishia watoa huduma kwa watoto njiti vyenye thamani ya shilingi
milioni 22. 19 kutoka shirika lisilo la kiserikali GIZ la Ujerumani ili kuweza
kutoa huduma bora katika kuwakuza watoto
hao kwa uangalifu wa hali ya juu na kwenye mazingira mazuri.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya mtoto
njiti duniani yaliyofanyika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema msaada wa vifaa hivyo
utaboresha huduma kwa watoto njiti.
“Kutokana na msaada wa vifaa hivyo naamini rufaa
zitapungua kwa kiasi kikubwa na kufanya huduma hizo kutolewa kwenye zahanati
zitazopelekewa vifaa hivyo “ alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa watumishi wa afya
ambao wamepata mafunzo wanatakiwa kuwaangalia wamama wanaotaka kujifungua ili
kuweza kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto nchini.
Mbali na hayo Dkt. Ulisubisya amesema kuwa wamama
wajawazito wanatakiwa kuhudhuria kliniki mara kwa mara pindi wanapopata
ujauzito ili kuweza kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ili kuepuka
kuzaa watoto njiti.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dkt. Wedson
Sichalwe amesema kuwa anashukuru Shirika la GIZ kwa mafunzo pamoja na vifaa vya
kutolea huduma kwa watoto njiti katika mkoa wake ili kutoa huduma bora kwa
watoto hao.
“Tumepata msaada mkubwa sana kwa mkoa wetu kwani
tulikua tunakabiliwa na changamoto za vifaa vya vya kuhudumia watoto njiti
wanaozaliwa katika zahanati na hospitali mkoani kwetu” alisema Dkt. Sichalwe.
No comments:
Post a Comment