Habari za Punde

AIRTEL 'INAPENDEZA' ZAIDI KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU,YAONGEZA GB ZA INTERNET, YABORESHA HUDUMA ZA UNI

 Bando mpya za Smatika na Yatosha kutoka mtandao wa Airtel zikiwa splaid wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuonyesha ongezeko la GB na kwa bei nafuu tofauti na awali ikiwa ni pamoja na maboresho ya huduma UNI iliyo boreshwa na jinsi ya kuipata.
Meneja Masoko wa Kampuni ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Anneth Muga, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo mchana.
********************************************
·       KAMPUNI ya Airtel Tanzania leo imekutana na wamiliki wa mitandao ya Kijamii na watangazaji mbalimbali wa Redio kwa lengo la kutoa ufafanuzi kuhusu maboresho ya huduma zao baada ya uzinduzi wa Bando mpya ya 'SMATIKA'.
Akizungumza katika mkutano huo Meneja Masoko wa Airtel, Anneth Muga,amesema kuwa Baada ya uzinduzi wa Bando la SMATIKA, baadhi ya wateja wameonekana kukwama kupata huduma za baadhi ya bando kama walivyozoea pamoja na kwamba kumekuwepo na matangazo ya mara kwa mara ya jinsi ya kupata huduma hizo na hasa bando la UNI.
Aidha, Anethy , amesema kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja kujichagulia bando la intaneti litakalompatia GB nyingi na muda wa maongezi wakati wowote, na kwa gharama nafuu ya hadi sh. 200 inayompa MB 40 ambayo haipatikani katika mtandao mwingine wowote.

 Meneja Uhusiano wa Airtel,  Jackson Mmbando ameongeza kufafanua kuwa kutokana na Airtel kutambua umuhimu wa matumizi ya Internet wameamua kuongeza ukubwa wa GB za matumizi ili kuwarahisishi wateja wao kufanya kazi bila hofu wala kubania DATA.
''Kwa sasa Bando mpya ya SMATIKA inampatia mteja GB 2 kwa siku saba kwa Sh. 5000, tofauti na ya awali iliyokuwa na GB 1,
Sh. 10,000 zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7 mpya ya sasa unapata GB 6 kwa siku saba. amesema Mbando

3 comments:

  1. Hakika GB hizi zinapendeza źaidi

    ReplyDelete
  2. Kiukwe inapendeza zaid, upande wa MB mmenikosha sana

    ReplyDelete
  3. Mimi kwangu mbona ni tofauti, wk moja nyuma ilikua UNI 500 ni GB 1.2 masaa 25, 1,000 GB 2 siku 3 lkn sahizi 1,000 ni mb 500 dah Airtel mtaniua jamani nioneeni huruma hata mm peke yangu tu

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.