Habari za Punde

MSIBA WA WAFANYAKAZI WATANO WA AZAM, SALIMU AZIKWA DAR LEO

 Msafara wa magari yaliyobeba miili ya wafanyakazi watano wa Azam Medi, ukiingia ofisi za Azam Tabata leo asubuhi kwa ajili ya shughuli za kuaga miili hiyo, ambapo baada ya shughuli hiyo Salim Mhando alizikwa katika makaburi ya Friends Corner  Manzese. Pumzikeni kwa amani wapiganaji wetu katika Tasnia ya Habari Ameen.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakiwa na huzuni getini wakisubiri kupokeza miili ya waliokuwa wafanyakazi wenzao.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakiwa na baadhi ya viongozi wakisimama kupokea miili ya marehemu ilipowasili kwenye viwanja vya Azam.
 Majonzi na vilio vilitawala mahala hapo....
 Waombolezaji kwenye viwanja vya Azam.
 NYUBANI KWA WAZAZI WA MAREHEMU SALIMU FRIENDS CORNER MANZESE.
Baadhi ya wachezaji wa Wahenga Fc wakiwa nyumbani wa marehemu Salimu wakishiriki shughuli za maziko.
 Kuelekea makaburini kwa maziko..

Wakijipanga kupokea jeneza....

 Waumini wa dini ya Kiislamu wakimswalia marehemu Salimu Msikiti wa Manzese Friends Corner.
Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya mwisho ya Salimu Mhando........

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.