Habari za Punde

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimwongoza mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Afrika Kusini zikipigwa katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akikagua Gwaride la Heshma aliloandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakipunga mkono kwa wananchi wakati wakielekea kwenye mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kabla ya kumpa zawadi ya Kinyago cha mpingo Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia zawadi ya picha aliopewa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika mazungumzo na mke wa Rais wa Afrika Kusini Dkt. Tshepo Motsepe-Ramaphosa baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi ya Picha mke wa Rais wa Afrika Kusini Dkt. Tshepo Motsepe-Ramaphosa baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Afrika Kusini Dkt. Tshepo Motsepe-Ramaphosa (kushoto) akimshukuru Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli baada ya kupokea zawadi ya picha Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.