Habari za Punde

WAREMBO, WASANII WACHANGAMKIA FURSA YA MAONESHO YA SADC

 Miss Tanzania 2008, Nasreen Karim, akimpiga picha mrembo namba tatu wa 2005, Sophia Byanaku, wakati walipokutana katik maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Msanii wa kuchora, Amani Grem, akiandaa sanaa yake ya Picha za Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alizochora kwa kutumia Shanga za rangi, aliposhiriki katika maonesho ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC katika Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zilishiriki.
Mabanda ya wafanyabiashara wa Vinyago yakiwa pembezoni mwa barabara ya Samora Avenue ikiwa ni maalumu kwa ajili ya maonesho na biashara kwa wageni washiriki wa Mkutano Mkuu wa 39 nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam, unaotaraji kuanza Agosti 17 na kumalizika 18.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.