Mfanyakazi wa Phoenix Tanzania Assurance Co. Ltd, akipiga picha na mtoto wa Kituo cha watoto Yatima Hisani, wakati walipowatembelea na kutoa msaada wa Chakula, Vifaa vya Shule, Nguo na Pesa Taslimu, ambapo pia walikula nao chakula cha mchana na kufurahi pamoja.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Phoenix Tanzania (Assurance Co. Ltd) Mubaraka Kibarabara (kushoto) amkimkabidhi sehemu ya msaada wa Chakula, Nguo, Vifaa vya Shule na Fedha Taslimu, Mkuu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatimba cha Hisani, Hidaya Mtalemwa, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipofika kutembelea kituo hicho kilichopo Mbagala Maji Matitu, Dar es Salaam, juzi kutoa msaada. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni hiyo, Godfrey Badeleya. (Picha Zote na Mafoto Media)
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Phoenix Tanzania (Assurance Co. Ltd) Mubaraka Kibarabara (kushoto) amkimkabidhi sehemu ya msaada wa Chakula, Nguo, Vifaa vya Shule na Fedha Taslimu, Mkuu wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatimba cha Hisani, Hidaya Mtalemwa, wakati
wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipofika kutembelea kituo hicho kilichopo Mbagala Maji Matitu, Dar es Salaam, juzi kutoa msaada. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni hiyo, Godfrey Badeleya. (kushoto) ni Meneja wa Phoenix, Robert Kalegeya.
Meneja akizungumza na watoto
Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni hiyo, Godfrey Badeleya, akizungumza
Na Mafoto Media
KAMPUNI ya Bima ya Phoenix of
Tanzania Assurance Co. Ltd, imejiwekea mkakati wa kusadia watoto Yatima kila
mwaka ili kuweza kusaidia na kuendeleza vipaji vya watoto waweze kufikia
malengo yao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Rasilimali watu wa Kampuni hiyo, Mubaraka
Kabarabara, wakati akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya Elimu, Chakula,
Nguo na Pesa taslimu, walipotembelea katika Kituo cha kulelea watoto Yatima cha
Hisani kilichopo Mbagala Maji Matitu jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Kabarabara alisema kuwa msaada huo
uliokabidhiwa katika Kituo hicho, ulichangwa na wafanyakazi wa Kampuni hiyo
baada ya mmoja wao kuwasilisha wazo na kujadiliwa kwa pamoja na kisha kufanyiwa
kazi mpaka kukamilika kwa zoezi hilo.
''Lilikuwa ni wazo la mmoja wetu aliyewasilisha kwetu na baada ya kujadiliana
ni jinsi gani tufanye ili kulifanyia kazi, tulikubaliana na kuweza kupata
michango ya wafanyakazi na kujadili vitu muhimu vya kuwasaidia watoto hawa na
kuwa na makubariano ya pamoja na ndiyo maana
hii leo tumeweza kulifanikisha zoezi hili,
Lakini pia baada ya kujionea na kutambua mahitaji ya watoto hawa bado ni mengi
na muhimu tumejiwekea utaratibu wa angalau kila mwaka tuwe tukifanya zoezi kama
hili hata mara moja ila tukifanikisha zaidi angalau tuweze kufanya hivi kna
kufurahi na watoto mara mbili kwa mwaka. alisema Kabarabara
Mwishoni mwa wiki Wafanyakazi wa Kampuni ya Phoenix walifika katika Kituo hicho
na kukabidhi msaada, ambapo pia walipata fursa ya kula chakula cha mchana
pamoja na watoto wa kituo hicho cha Hisani chenye jumla ya watoto 75.
Akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Phoenix, Mkuu wa Kituo hicho, Hidaya
Mutalemwa, aliwashukuru wadau wa Kampuni ya Phoenix waliojitolea kufika na
kutoa msaada kwa watoto wa kituo hicho chenye changamoto nyingi ambazo kuisha
kwake kunategemea wadau mbalimbali.
''Hatuna neno zuri la kusema ili mtuelewe tunawashukuru kwa kiasi gani,
ila mungu awabari kwa hiki mlichokitoa kwa watoto wetu leo wamefurahi kiasi
wengine wanawalilia msiondoke muendelee tu kubaki nao, Changamoto ni nyingi
katika kituo hiki ambazo nyingi zinategemea wadau kama ninyi ili watoto
waendelee kuishi kwa amani na furaha kama hii leo''. alisema Hidaya.
Picha ya pamoja....
No comments:
Post a Comment