Habari za Punde

WACHEZAJI SIMBA WAKABIDHIWA BODA BODA ZAO

 Nahodha wa Simba, John Bocco, na Erasto Nyoni, wakifurahia jambo wakati wakijaribu Pikipiki baada ya kukabidhiwa katika hafla fupi ya kukabidhi Pikipiki kwa wachezaji wa Simba wa Msimu uliopita ikiwa ni ahadi ya Mfadhili wa Klabu hiyo, Mo Dewji. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, leo mchana. 
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL, Fatma Dewji (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa funguo ya Pikipiki aina ya Boxer, Nahodha wa Simba, John Bocco, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Pikipiki kwa wachezaji wa Simba wa Msimu uliopita ikiwa ni ahadi ya Mfadhili wa Klabu hiyo, Mo Dewji. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Simba, Senzo Mazingiza (wa pili kulia) ni Kocha, Patrick Aussems.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL, Fatma Dewji (wa tatu kulia) akimkabidhi mfano wa funguo ya Pikipiki aina ya Boxer, mchezaji wa Simba, Rashid Juma, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Pikipiki kwa wachezaji wa Simba wa Msimu uliopita ikiwa ni ahadi ya Mfadhili wa Klabu hiyo, Mo Dewji. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia (mbele) ni Ofisa Mtendaji, Senzo Mazingiza na baadhi ya wachezaji na Viongozi wa Klabu hiyo.  
 Nyoni akijaribu kuvaa Kofia ngumu
Nyoni akionesha funguo baada ya kukabidhiwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.